KAYA 7,775,181 ZINA VYOO BORA
TANZANIA
Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 kaya zenye vyoo bora zimeongezeka hadi kufikia kaya 7,775,181 sawa na 77.5% ikilinganishwa na kaya 7,087,523 sawa na 73.2% zilizokuwa na vyoo bora katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23.
Hili ni sawa na ongezeko la kaya 687,658 sawa na 4.3% katika kipindi cha mwaka mmoja.
Lengo la serikali ni kufikia 85% ifikapo mwaka 2025, hivyo jitihada zinaendelea ili kuweza kufikia shabaha iliyojiwekea.