VIJANA 10,220 WAPEWA MAFUNZO YA UKUZAJI UJUZI
TANZANIA
Mwaka 2023, Serikali imeendelea kutekeleza Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi kwa vijana kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira mabapo jumla ya 10,220 wamepata mafunzo ya ujuzi unaohitajika katika soko la ajira ili waweze kuajiriwa na kujiajiri ikilinganishwa na vijana 21,586 waliopata mafunzo mwaka 2022.
Kati ya hao, vijana 4,273 walipata mafunzo ya uanagenzi (ufundi stadi vyuoni, uchumi wa buluu, unenepeshaji wa mifugo na Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora - BBT), wafanyakazi 1,593 wa sekta ndogo ya utalii na ukarimu pamoja na wafanyabiashara wadogo na wa kati walipata mafunzo ya kukuza ujuzi na wahitimu 4,354 walipata mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi.