UZALISHAJI MAZAO MAKUU YA CHAKULA WAONGEZEKA

 

UZALISHAJI MAZAO MAKUU YA CHAKULA WAONGEZEKA

UZALISHAJI MAZAO MAKUU YA CHAKULA WAONGEZEKA

TANZANIA.
Mwaka 2023, uzalishaji wa mazao makuu ya chakula umeongezeka kwa 19.0% na kufikia tani 20,402,014 ikilinganishwa na tani 17,148,290 mwaka 2022. 
Kati ya hizo, tani 11,448,757 zilikuwa za mazao ya nafaka na tani 8,953,258 mazao yasiyo ya nafaka. 
Ongezeko la uzalishaji lilichangiwa na kuwepo kwa mvua za kutosha katika maeneo mengi ya uzalishaji, kuimarika kwa huduma za ugani na upatikanaji wa vitendea kazi, matumizi ya teknolojia na pembejeo bora za kilimo ikiwemo mbegu na mbolea na kuimarika kwa usimamizi wa upotevu mazao kabla na baada ya kuvuna. 
Katika kipindi hicho, mahitaji ya chakula yalikuwa tani 16,390,404 ikilinganishwa na tani 15,053,034 mwaka 2022 na hivyo kuwa na ziada ya chakula ya kiasi cha tani 4,011,611. Kulingana na mahitaji ya chakula, nchi ilikuwa na kiwango cha utoshelevu wa chakula wa 124.5%.