RUAHA WAJENGEWA KIWANJA KIPYA CHA NDEGE

 

RUAHA WAJENGEWA  KIWANJA KIPYA CHA NDEGE

RUAHA WAJENGEWA  KIWANJA KIPYA CHA NDEGE 

MBEYA
Kiwanja kipya cha ndege cha Shilingi milioni  780 kimejengwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha katika Kijiji cha Mlungu, Wilaya ya Mbarali jijini Mbeya ili kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili haramu na kuvutia watalii zaidi.
Kiwanja hicho cha ndege kimefunguliwa rasmi jumatatu (juni 24, 2024) ambapo kiwanja hicho cha ndege kimejengwa wakati muafaka kikikamilisha juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya utalii, hasa chini ya mpango wa Usimamizi wa Maliasili kwa Utalii na Ukuaji (REGROW).
Kiwanja hicho kina  barabara ya kurukia ndege ya changarawe yenye urefu wa kilomita 1.2, jengo la kituo lenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 30. 
Aidha kiwanja hicho kitasogeza fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka Ruaha kutokana na idadi ya watalii inayotarajiwa kupanda.