MHE.RAIS SAMIA ATOA NDENGE KUSAFIRISHA MWILI WA RAS

 

MHE.RAIS SAMIA ATOA NDENGE KUSAFIRISHA MWILI WA RAS

MHE.RAIS SAMIA ATOA NDENGE KUSAFIRISHA MWILI WA RAS

KILIMANJARO
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametoa ndege maalum iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (RAS), Dk. Tixon Nzunda (56), kwenda nyumbani kwake Goba, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi, ofisi ya makamu wa Rais imesema kwa niaba ya Mhe Rais Dkt Samia.
Mwili huo umesafirishwa kwa ndege maalum iliyotolewa na Dkt Samia kuelekea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam (Goba), kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). 
Aidha Dk. Nzunda na dereva wake, Alphonce Edson (54), walipoteza maisha Juni 18, mwaka huu, saa 8:30 mchana katika eneo la Mjohoroni (Palestina), Kata ya KIA, Wilaya ya Hai, baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser VXR, kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lililokuwa likitokea Arusha kwenda Moshi na maziko yanatarajiwa kufanyika Juni 22, 2024  Jijini Dar es salaam.