MTO RUHUHU KUZALISHA UMEME MW 321

 

MTO RUHUHU KUZALISHA UMEME MW 321

MTO RUHUHU KUZALISHA UMEME MW 321 

RUVUMA
Mradi wa Kuzalisha Umeme  (MW 321) kwa Kutumia maporomoko ya maji ya mto Ruhuhu mkoani Ruvuma pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kiloviti 220 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka Kikonge hadi kituo cha kupoza umeme cha Madaba upo mbioni kuanza katika mkoa wa Ruvuma.
Serikali inaendelea na utaratibu wa kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na kukamilisha taarifa muhimu za mradi ikiwemo tathmini ya kina ya Athari za Kijamii na Mazingira (detailed ESIA), uwekaji wa mipaka katika eneo la uzalishaji wa umeme, usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni za mradi (bwawa la kuzalisha umeme na njia ya kusafirisha umeme).
Aidha, maandalizi ya kufanya tathmini katika eneo la bwawa la uzalishaji umeme yameanza. 
Vilevile, hatua za awali za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kazi za Mazingira zinaendelea.