TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MASHINDANO YA MATAIFA 8
TANZANIA
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano mapya ya soka ya wanawake ya timu yaliyoandaliwa na Shirika la Homeless WorldCup yatakayofanyika juni 29 na 30 mwaka huu Mkoani Arusha.
Mbali na Tanzania mwenyeji, timu zilizothibitishwa kushiriki ni pamoja na Kenya, Malawi, Afrika Kusini, Namibia, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Aidha Mashindano hayo yatafanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) eneo la Kijenge, mkabala na makutano ya mzunguko wa Impala, kando ya barabara ya Njiro.
Mashindano hayo mapya yanaanzishwa ili kuimarisha kujitolea kwa Wakfu wa Kombe la Dunia la Wasio na Makazi kukuza mchezo wa Wanawake kote ulimwenguni pia lengo lingine ni kuelimisha na kusaidia Nchi Wanachama wa Afrika katika kuendeleza mchezo huo zaidi nchini kote, pamoja na kuwawezesha wanawake.