TSH BIL 97.13 ZILIENDA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI
TANZANIA
Kwa mwaka wa fedha 2023/24 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ( National Audit Office-NAOT) iliidhinishiwa matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 97.13.
Kati ya kiasi hicho, matumizi ya kawaida shilingi bilioni 87.72 na matumizi ya maendeleo shilingi bilioni 9.41.
Matumizi ya kawaida yanajumuisha matumizi mengineyo shilingi bilioni 70.83 na mishahara shilingi bilioni 16.89.
Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuisha fedha za ndani shilingi bilioni 8.83 fedha za nje shilingi milioni 583.88.