TSH BIL 5.2 KUENDELEZA BARABARA TARIME – MUGUMU (KM 86.05)

TSH BIL 5.2 KUENDELEZA BARABARA  TARIME – MUGUMU (KM 86.05)

TSH BIL 5.2 KUENDELEZA BARABARA  TARIME – MUGUMU (KM 86.05)

MARA
Jumla ya Shilingi bilioni 5 na milioni 200  zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara za Mogabiri – Nyamongo (km 25) na Tarime – Mogabiri (km 9.3), Nyamongo – Mugumu (km 48.15) pamoja na barabara ya kuelekea Mugumu Roundabout (km 3.6).
 Kazi nyingine ni kuanza ujenzi wa barabara ya Mika – Utegi – Shirati – Kirongwe (km 56.8); Sehemu ya Mika – Utegi – Shirati (km 27).