MHE RAIS SAMIA AHUDHURIA UAPISHO WA MHE.RAMAPHOSA
AFRIKA KUSINI.
Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo juni 19 amehudhuria Hafla ya uapisho wa Rais Mteule (ambae kwa sasa tayari ni Rais ) Cyril Ramaphosa nchini Afrika kusini uliofanyika katika Viwanja vya Jengo la Umoja, Pretoria nchini humo.
Sambamba na Mhe Rais Samia kutoka Tanzania wakuu wa nchi za Liberia,Namibia, Nigeria, Kenya, Mauritius, Mauritania, Comoros, DRC, Madagascar, Botswana, Msumbiji, Misri, Togo,Rwanda,Uganda, Senegal,Angola na pamoja na mfalme Mswati wa III kutoka Eswatini na Letsie wa III kutoka Lesotho wameshiriki kwenye hafla hiyo ya uapisho.
KUMBUKA:- Dkt Samia ameondoka nchini (jana jioni) Juni 18 na kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ziara ya siku moja kwa ajili ya kushiriki shughuli ya uapisho (ambao umefanyika leo juni 19, 2024).