TSH BIL 25 ZAKAMILISHA KITUO CHA KUPOZEA UMEME

 

TSH BIL 25 ZAKAMILISHA KITUO CHA KUPOZEA UMEME

TSH BIL 25 ZAKAMILISHA KITUO CHA KUPOZEA UMEME 

MOROGORO
Tanzania imezindua rasmi kituo cha kuzalisha umeme cha 20MVA cha Ifakara kilichokamilika kwa  Dola za Marekani milioni 9.6 (takriban shilingi bilioni 25) katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambacho kinatarajiwa kuongeza nguvu katika kuimarisha upatikanaji wa umeme  kwa wakazi na wafanyabiashara.
Kituo hicho  kitahudumia wakazi wa wilaya tatu za Malinyi, Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro pia kituo hicho kipya kitabadilisha kwa kiasi kikubwa uchumi wa wananchi katika eneo hilo, viwanda vya kuzalisha umeme na huduma za kijamii.