2025 VIJIJINI MAJI SAFI YATAPATIKANA KWA 85%
TANZANIA
Lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuwapatia wananchi waishio vijijini huduma ya majisafi na salama kufikia zaidi ya 85% ifikapo mwaka 2025.
Katika kutimiza lengo hilo, Serikali imeendelea kujenga, kukarabati, kupanua mitandao ya kusambaza maji pamoja na kuimarisha usimamizi wa huduma ya maji.
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka wastani wa 74.5% mwezi Desemba, 2021 hadi kufikia wastani wa 77% mwezi Desemba, 2022.
Kiwango kilichoongezeka kimetokana na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi 586 yenye vituo 5,748 vya kuchotea maji vinavyonufaisha wananchi wapatao 4,086,442 kwenye vijiji 1,293.
Hali hiyo, inafanya jumla ya wananchi wa vijijini wanaopata huduma ya maji kuwa 30,209,409
