TSH BIL 12 KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI

 

TSH BIL 12 KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI

TSH BIL 12 KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI

DODOMA
Serikali ya awamu ya sita imetenga kiasi cha shilingi bilioni 12 katika utekelezaji wa mradi wa kulifanya Jiji la Dodoma kuwa la kijani.
Kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kupanda miti na maua katika hifadhi za barabara ili kutunza mazingira na kupendezesha mandhari ya jiji hilo
Mradi huo wa Green Solution Project (GSP) unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ambayo pia  inafadhili mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilometa 112.3
Kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo katika jiji la Dodoma utafungua mawanda mapana kwa serikali kutafuta wadau wa maendeleo watakaoshirikiana nayo kukijanisha maeneo mbalimbali nchini.
Serikali ina mpango wa kukutana na wamiliki na wawekezaji wa maeneo yaliyo pembezoni mwa barabara ili kuweka mkakati wa pamoja wa upandaji miti na bustani za maua ili kuendelea kukijanisha nchi.