DKT SAMIA AKABIDHIWA TAARIFA(TUME YA HAKI JINAI)
DODOMA
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Juni 15, 2024 amepokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Sefue katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.