SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA TSH BIL 637

 

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA  TSH BIL 637

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA  TSH BIL 637 

DAR ES SALAAM
Kiasi cha Shilingi bilioni 637 zimeingizwa kwenye hazina ya serikali kama gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma ambayo serikali ni mbia, katika hafla iliyoshuhudiwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Juni 11, 2024 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Kati ya hizo, shilingi bilioni 279 zimetoka kwa makampuni ya biashara, wakati shilingi bilioni 358 zilizobaki ni michango kutoka kwa taasisi nyingine za umma.
Taarifa kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) imesema  fedha hizo zimekusanywa kuanzia Julai 2023 hadi Mei 2024, ambapo jumla ya shilingi bilioni 850 zinatarajiwa kukusanywa mwishoni mwa mwezi huu.
"Natoa wito kwa wale wanaodaiwa fedha, wale ambao wamefanya malipo ya sehemu, na wale ambao hawajachangia kabisa wahakikishe wanakamilisha malipo yao kwa mwaka huu wa fedha," imesema taarifa kutoka TR
Miongoni mwa wachangiaji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeongoza kwa kupata shilingi bilioni 153.91,  Benki ya NMB yenye shilingi bilioni 57.392, madini ya Twiga yenye shilingi bilioni 53.4, Airtel Tanzania  bilioni 40.8, Puma Energy sh 12.2  na TPC Moshi sh bilioni  10.2.
Michango mingine mikubwa imetoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye Shilingi bilioni 34, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  Sh. bilioni 21.3, Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) shil.bilioni 19.1 na BRELA shilingi bilioni 18.9.