MV MAGOGONI KUKAMILIKA DISEMBA 2024
DAR ES SALAAM
Ukarabati wa Kivuko cha Mv. Magogoni unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwezi Desemba, 2024 na kurejeshwa Nchini ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Lengo la ukarabati huo wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini, kuharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, na maeneo mengine Jijini Dar es salaam.
Itaumbukwa kuwa Mwezi Februari 2023 Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ilisaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.5.