DKT SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA MAKAMU, WENGINE 9 MALAWI

 

DKT SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA MAKAMU, WENGINE 9 MALAWI

DKT SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA MAKAMU, WENGINE 9 MALAWI

DAR ES SALAAM
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi  kwa Rais wa Malawi Lazarus Chakwera kufuatia kuondokewa na Makamu wa Rais Dk Saulos Chilima na wengine 9 waliofariki dunia kutokana na ajali ya ndege.
Kupitia mtandao wa X na instagram wa Mhe Rais @ SuluhuSamia ameandika” It is with great sadness that I have received the news of the tragic demise of the Vice President of the Republic of Malawi, the Right Honourable Dr. Saulos Klaus Chilima
On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, I convey our deepest condolences to His Excellency President @ LAZARUSCHAKWERA , the people of the Republic of Malawi, family and friends. May his soul rest in peace. Amen.”
“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa za kifo cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mheshimiwa Dkt. Saulos Klaus Chilima.
"Kwa niaba ya Serikali na Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu zetu za rambirambi kwa Mheshimiwa Rais @LAZARUSCHAKWERA, watu wa Jamhuri ya Malawi, familia na marafiki," Rais  Samia ameandika.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri nchini Malawi imeeleza kuwa ndege hiyo iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais Dk Saulos Chilima na wenzake tisa imekutwa asubuhi ya leo katika msitu wa Chikangawa na kuongeza kuwa “kwa bahati mbaya wote waliokuwemo wameangamia. katika ajali hiyo.”
Operesheni hiyo ya utafutaji na uokoaji iliyozinduliwa mara baada ya ndege hiyo kuruka kwenye rada, iliendeshwa na vyombo mbalimbali vikiwemo Jeshi la Ulinzi la Malawi, Jeshi la Polisi na Idara ya Usafiri wa Anga.
Aidha Kufuatia msiba huo Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza siku ya kitaifa ya maombolezo na ameagiza bendera zote zipepee nusu mlingoti kuanzia leo (Jumanne) hadi siku ya mazishi.
BimkubwaTanzania Tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kuwapa pole Rais wa Malawi, familia za marehemu na wananchi wote wa Jamhuri ya Malawi