SERIKALI KUKARABATI MAJENGO YA UTAWALA
GEITA
Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukarabati na kutunza majengo ya utawala katika halmashauri zote nchini ikiwemo Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita.
Ujenzi wa majengo hayo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020-2025, inayoielekeza Serikali kutoa miundombinu hiyo muhimu.