DKT SAMIA AONGEZA MTANDAO WA BARABARA ZA LAMI

 

DKT SAMIA AONGEZA  MTANDAO WA BARABARA  ZA LAMI

DKT SAMIA AONGEZA  MTANDAO WA BARABARA ZA LAMI

TANZANIA
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ilipoingia madarakani Machi, 2021, mtandao wa barabara za lami ulikuwa kilometa 10,830.2 ambapo  hadi kufikia Machi, 2024, mtandao wa barabara za lami umeongezeka na kufikia kilometa 12,028.7 ikiwa ni ongezeko la kilometa 1,198.50 za lami.
Ongezeko hili linatokana na kukamilika kwa miradi ya barabara 25 zenye jumla ya kilometa 1,198.50. 
Aidha Kukamilika kwa barabara hizo kumechangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mawasiliano, kuimarisha biashara pamoja na kukuza uchumi wa maeneo husika.