DKT SAMIA AWAMWAGIA TEMESA TSH BIL 74.2+

 

DKT SAMIA AWAMWAGIA  TEMESA TSH BIL 74.2+

DKT SAMIA AWAMWAGIA  TEMESA TSH BIL 74.2+  

DODOMA
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) wamekiri kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi 67,723,669,720.20 ikiwa inajumuisha ujenzi na ukarabati wa karakana, ujenzi wa vivuko na maegesho ya vivuko.
Pia Serikali ya awamu ya sita imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 7.2 ambazo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa karakana mpya na ukarabati ambapo Mkoa wa Dodoma ni mojawapo ya mnufaika wa fedha hizo kwa kuwa Serikali kupitia TEMESA imeanza mchakato wa usanifu wa karakana hiyo ya kisasa ambayo itajengwa katika maeneo ya Kizota Mkoani Dodoma ujenzi utakapokamilika itaweza kuhudumia magari yote ya Taasisi za Serikali Mkoani Dodoma kwa ufanisi mkubwa.