W/UCUHUKUZI 202324 ILIIDHINISHIWA TSH TRIL 2.089

 

WUCUHUKUZI 202324 ILIIDHINISHIWA TSH TRIL 2.089

W/UCHUKUZI 2023/24 ILIIDHINISHIWA TSH TRIL 2.089

DODOMA
Katika mwaka wa fedha 2023/24, Wizara ya Uchukuzi (Fungu 62) iliidhinishiwa jumla ya Shilingi Trilioni 2.089 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. 
Kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni 118.215 ni za Matumizi ya Kawaida ya Wizara na Taasisi zake na Shilingi Trilioni 1.971 ni za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Hadi kufikia Machi, 2024 Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi Trilioni 1.827 sawa na asilimia 87.48 ya bajeti yote ya Wizara iliyoidhinishwa.
Kati ya fedha hizo zilizopokelewa, Shilingi Bilioni 71.125 ni fedha Za Matumizi ya Kawaida ambazo ni sawa na 60.16% ya bajeti ya Matumizi ya Kawaida iliyoidhinishwa, na Shilingi Trilioni 1.756 ni fedha za Miradi ya Maendeleo ambazo ni sawa na a
89.12% ya bajeti ya Maendeleo iliyoidhinishwa. 
Baada ya kupokea fedha hizo, Wizara ya Uchukuzi iliendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kimkakati