TSH BIL 15 ZAIMARISHA UGANI NCHINI

 

TSH BIL 15 ZAIMARISHA UGANI NCHINI

TSH BIL 15 ZAIMARISHA UGANI NCHINI

TANZANIA
Jumla ya Shilingi Bilioni 15 zilitengwa na serikali awamu ya sita katika bajeti ya mwaka 2023/2024 kwa ajili ya kuimarisha huduma za ugani nchini.
Kazi zilizopangwa katika mwaka 2023/2024 ni kununua na kusambaza magari 55, visanduku vya ugani 4,000, sare 4,000, soil scanner 45 na vishikwambi 1,500 na kusambaza kwa maafisa ugani ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za ugani kwa wakulima.
Aidha hadi Aprili, 2024 Wizara ya kilimo imenunua vishikwambi 4,446 sawa na 296.4% ya lengo. 
Kati ya hivyo vishikwambi 946 vimesambazwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu na taarifa za kilimo (ARDS) na usambazaji unaendelea.