DKT SAMIA AKITA MIZIZI KWENYE ELIMU.

 

DKT SAMIA AKITA MIZIZI KWENYE ELIMU.

DKT SAMIA AKITA MIZIZI KWENYE ELIMU.

DODOMA
Katika mwaka wa fedha 2023/24 Bunge liliidhinisha shilingi   trilioni 1.7 kwa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku mwaka 2022/23 wizara  hiyo ikiidhinishiwa bajeti ya shilingi trilioni 1.5
Katika kuhakikisha elimu inaongeza nguvu zaidi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  siku za hivi karibuni imetoa bajeti yake ya mwaka 2024/2025 kiasi cha shilingi trilioni 1.97 ikiainisha maeneo matano ya kipaumbele yanayolenga kuboresha ubora wa elimu kwa vijana wa Kitanzania.
Pia Serikali itajikita katika kuongeza fursa na kuboresha ubora wa mafunzo ya elimu ya ufundi stadi, kuongeza fursa na ubora katika elimu ya msingi, sekondari na vyuo vya ualimu, kupanua fursa na ubora katika vyuo vya elimu ya juu, na kuimarisha utafiti, sayansi, teknolojia; na mipango ya uvumbuzi