WANAOSAFIRI KWA ANGA WAONGEZEKA
DAR ES SALAAM
Hadi kufikia Machi, 2024 abiria waliosafiri kwa kutumia usafiri wa anga wameongezeka hadi abiria 5,080,920 ikilinganishwa na abiria 4,105,375 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2022/23, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 23.76. (Hii ni kwa mujibu wa wizara ya uchukuzi via TCAA)
Vilevile, mizigo iliyosafirishwa imeongezeka hadi kufikia tani 27,532 ikilinganishwa na tani 23,070.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 19.33.
