BANDARI 45 ZARASIMISHWA

 

BANDARI 45 ZARASIMISHWA

BANDARI 45 ZARASIMISHWA

DAR ES SALAAM
Serikali kupitia TASAC katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Machi, 2024 imerasimisisha bandari bubu zipatazo 45  za Tanzania Bara kati ya 99  zilizokaguliwa na kufanyiwa tathmini ya kina na serikali.
Lengo la hatua hii ni kuhakikisha kuwa Serikali inaimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya bandari ili kuboresha utoaji wa huduma.
Aidha Serikali kupitia TASAC imeendelea kutoa leseni na vyeti vya usajili kwa watoa huduma waliokidhi vigezo ambapo hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya watoa huduma 1,722 walisajiliwa na kupewa leseni ikilinganishwa na jumla ya watoa huduma 1,498 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la 14.95%