WAKAZI WA KIBADA-MWASONGA MNAWEKEWA LAMI

WAKAZI WA KIBADA-MWASONGA MNAWEKEWA  LAMI

WAKAZI WA KIBADA-MWASONGA MNAWEKEWA  LAMI

DAR ES SALAAM
Serikali tayari imeshampata Mkandarasi na kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Kibada – Mwasonga – Kimbiji yenye urefu wa kilometa 41 kwa kiwango cha lami.
Aidha Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongezwa kwa ujenzi wa kilometa 10 katika barabara hiyo ya Kibada – Mwasonga – Kimbiji kwa kuiunganisha na kipande kilichobakia cha Kimbiji hadi Cheka kwa kiwango cha lami.