MAAFISA TARAFA 63 WAAJIRIWA
TANZANIA
katika mwaka 2023/24 serikali ya awamu ya sita imeajiri maafisa tarafa 63 na kupangiwa vituo vya kazi kati ya nafasi wazi 84.
Aidha, katika kuboresha utendaji kazi, umefanyika msawazo wa watumishi wa halmashauri zilizokuwa na watumishi wengi na kuwahamishia halmashauri zenye upungufu wa watumishi ambapo watumishi 646 walihamishwa.
Aidha serikali kupitia OR– TAMISEMI inakamilisha taratibu za kuajiri watendaji wa kata 525, watendaji wa vijiji 1,986, watendaji wa mitaa 1,333 na maafisa tarafa 21.
