TSH BIL 73.5 KUBORESHA KIWANJA CHA NDEGE MTWARA
MTWARA
Jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 73.5 kitatumika kujenga jengo la Abiria, Vituo vya Zimamoto na Hali ya Hewa, Pamoja na Mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mtwara.
Kuelekea utekelezaji wa zoezi hilo, April 29, 2024 serikali kupitia wizara ya uchukuzi imesaini Mkataba wa usanifu na ujenzi wa jengo la Abiria, Vituo vya Zimamoto na Hali ya Hewa, Pamoja na Mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege hicho ambapo mkataba huo umesainiwa baina ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group(CRCEG )kutoka China na utatekelezwa kwa miezi 36.
ZINGATIA:- JENGO HILO LITAKAPOKAMILIKA LITAKUWA NA UWEZO WA KUHUDUMIA ABIRIA MILIONI MOJA KWA MWAKA.
