UJENZI MRADI WA SOKO (LOT 1&3) WAKAMILIKA

 

UJENZI  MRADI WA SOKO (LOT 1&3) WAKAMILIKA

UJENZI  MRADI WA SOKO (LOT 1&3) WAKAMILIKA

DODOMA
SERIKALI kupitia   Wizara ya Kilimo chini ya mradi wa TANIPAC imekamilisha utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Soko (Lot 1) na Kituo cha Uhaulishaji Teknolojia (Lot 3) wilayani Kongwa Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya Kituo Mahiri cha Usimamizi wa Mazao ya Nafaka Baada ya Kuvuna na ujenzi huo umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi 10,762,683,129.25.
Kituo hiki kinakwenda kumnufaisha mkulima, kutengeneza ajira na ndani ya kituo hiki kuna kituo maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana na wanawake kwenye teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao yetu ya nafaka
Aidha serikali kupitia Wizara ya kilimo inaendelea na utekelezaji wa ajenda 10/30 ambapo moja ya mikakati ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 Tanzania iweze kuhifadhi angalau tani million 3 za chakula, huku kupitia kituo hicho kinakwenda kuhifadhi karibu tani 20,000.