WACHIMBAJI WADOGO WANUNULIWA MASHINE
DODOMA
Kwa kutambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, seeikali kupitia Wizara ya madini imeliwezesha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kununua mitambo mitano (5) ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Mitambo hiyo tayari imeanza kazi ya uchorongaji kuanzia tarehe 4 Desemba, 2023 katika maeneo ya leseni za wachimbaji wadogo ya Nyamongo-Tarime, Itumbi-Chunya, LwamgasaGeita, Katente-Bukombe, Buhemba-Butiama na NholiDodoma
Aidha serikali kupitia STAMICO inakusudia kufanya ujenzi wa vituo vipya viwili vya mfano vya kuchakata madini ya chokaa na chumvi.
Kituo kwa ajili ya kuchakata madini ya chokaa kitajengwa katika eneo la Kona Z Mkoa wa Tanga na kituo kwa ajili ya kuchakata chumvi kitajengwa katika eneo la Nangurukuru-Kilwa.
