TSH BIL5.7 ZACHOCHEA UCHUMI CHALINZE
PWANI
Kiasi cha shilingi bilioni 5.7 kilichotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ghorofa tatu la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani kimeongeza ukuaji wa shughuli za uchumi katika eneo linalozunguka jengo hilo na kuongeza ari na morali ya utendaji kazi wa watumishi wa umma wa halmashauri hiyo
Kabla ya kukamilika kwa Jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, ofisi za halmashauri hiyo zilikuwa Lugoba katika nyumba ambazo waliazimwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na baada ya kukamilika watumishi na wananchi hivi sasa wanafurahia huduma katika jengo jipya la utawala la Chalinze kwani zamani walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma Lugoba.
