TSH BIL 54 KUCHIMBA VISIMA 900 MAJIMBO 180
MANYARA
Kiasi cha shilingi bilioni 54 kitatumika kwa ajili ya uchimbaji wa visima 900 kwenye majimbo 180 ya vijijini kwa visima vitano kwa kila jimbo kwenye maeneo hayo.
Kwa kuanza mpango huo serikali kupitia RUWASA imezindua zoezi hilo katika kijiji cha Maescron Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara kwa kuchimba kisima cha kwanza.
Utekelezaji wa mpango huo unategemea fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia programu ya P for R, Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) pamoja na Wadau mbalimbali.
KUMBUKA:- Utaratibu wa uchimbaji wa visima hivyo ni maelekezo ya Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake za kumtua mama ndoo kichwani.
