VIWANDA 28 HUZALISHA CHUMA NCHINI
TANZANIA
Tanzania ina jumla ya viwanda 28 vya kuzalisha chuma na bidhaa za chuma.Viwanda hivyo vipo katika makundi mbalimbali yanayojumuisha nondo, mabati, mabomba, misumari, senyenge na kadhalika.
Kati ya viwanda hivyo, 19 vinazalisha nondo na vina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 1,299,240 kwa mwaka na uzalishaji halisi ni tani 900,000 kwa mwaka sawa na 82.8% ya uwezo uliosimikwa.
Viwanda tisa vilivyosalia vinazalisha bidhaa nyingine za chuma.
Aidha, viwanda hivyo vimeajiri jumla ya wafanyakazi 25,358, kati ya hao wafanyakazi 4,169 ni ajira za moja kwa moja na wafanyakazi 21,189 wa ajira zisizo za moja kwa moja.
KUMBUKA:- KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2022 HADI MWAKA 2023, MATUMIZI YA BIDHAA ZA CHUMA NCHINI YAMEONGEZEKA KUTOKA TANI 1,000,000 HADI KUFIKIA TANI 1,200,000 KWA MWAKA, IKIWA NI ONGEZEKO LA 20%.
