VIWANDA 14 HUZALISHA SARUJI NCHINI
TANZANIA
Tanzania ina jumla ya viwanda vya saruji 14 ambapo viwanda vikubwa (intergrated plant) ni saba (7) na vilivyosalia saba (7) ni viwanda vidogo.
Kutokana na takwimu za uzalishaji wa saruji kwa mwaka 2023 ambazo zinaakisi hitaji la soko hasa matumizi ya saruji katika miradi mikubwa inaonesha kuwa, viwanda vya saruji nchini vilizalisha tani 9,107,973 za saruji kwa mwaka ambapo mahitaji ya ndani ya nchi ni takriban tani 8,000,000 kwa mwaka, hivyo, kuna ziada ya tani 1,107,973 ambayo huuzwa nje ya nchi
Viwanda hivyo huuza saruji katika nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia. Sekta hiyo imeajiri wafanyakazi 17,885 ambapo kati ya hao, wafanyakazi 4,176 ni ajira za moja kwa moja na wafanyakazi 13,709 ni ajira zisizo za moja kwa moja
