MIKOA INAYOLIMA MBEGU ZA MAFUTA YA KUPIKIA YAONGEZEKA
TANZANIA
Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji na hii imepelekea kuongezeka kwa Mikoa inayolima mbegu za mafuta ya kula nchini kutoka mikoa 15 hadi mikoa 19.
Mikoa iliyoongezeka ni Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Njombe.
Hali hii inatokana na uhamasishaji wa programu ya kujitosheleza kwa mafuta ya kula nchini ambapo mikoa yenye uwezo wa kulima mbegu za mafuta imehamasishwa na kuanza kilimo hicho.
Aidha, Serikali imeondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika mafuta yaliyosafishwa yanayozalishwa na viwanda vya ndani kwa lengo la kupunguza bei ya mafuta ya kula ili yaweze kushindana na mafuta yanayotoka nje ya nchi.
ZINGATIA:- katika mwaka 2022 Serikali ilifanya Mabadiliko ya Sheria ya Ushuru wa Forodha na kupunguza ushuru wa uagizaji wa mafuta ghafi ya chikichi (Crude Palm Oil) kutoka asilimia 25 hadi 0.
