"MAMA SAMIA MENTORSHIP PROGRAM’’ YAWAGUSA WATOTO 6,000
TANZANIA
Program ya kuendesha mafunzo elekezi kazini kwa huduma za Mama na Mtoto ijulikanayo kama “Mama Samia mentorship program kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, imefanikisha kuwafikia Mama na Mtoto 6,000 kutoka Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Lengo la mpango huo ni kuendelea kuimarisha ubora wa utoaji huduma za afya ya uzazi mama na mtoto stadi na ujuzi wa watoa huduma ili kupata matokeo chanya, mpango huu umetoa Mafunzo kwa wakufunzi ngazi ya vituo katika Mkoa wa Kigoma, Tanga, Dar Es Salaam, Mara na Kagera.
