VITUO 615 VYA KUJIFUNGULIA VYABORESHWA
TANZANIA
Katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea na ujenzi wa miundombinu ya maji safi, vyoo, mabafu, vifaa vya kunawia mikono, viteketezi taka (incinerators) na maboresho ya vyumba vya kujifungulia akina mama wajawazito kwenye Vituo 615.
Ujenzi wa miundombinu hii unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2024 ambapo itafikisha jumla ya vituo 2,517 ambavyo vimenufaika kupitia mradi wa SRWSS.
Hadi kufikia Machi 2024 utekelezaji wa miradi umefikia vituo 1902 sawa na asilimia 72.2 ya lengo la kufikia vituo 2,636 ifikapo Julai 2025.
