TSH BIL 28+ KUJENGA VITUO JUMUISHI (KILIMO)
IRINGA
Serikali kupitia Wizara ya kilimo katika mwaka wa fedha 2023/2024,ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 28.23 ili ijenge Vituo Jumuishi (common use facilities) vitatu (3) vya kukusanya, kuchambua, kupanga madaraja, kufungasha na kusafirisha mazao ya bustani katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Vituo hivyo, vitawezesha kupunguza upotevu wa mazao ya bustani, kuongeza ubora na mauzo ya mazao hayo ndani na nje ya nchi.
Hadi Aprili, 2024 mkataba wa ujenzi wa vituo jumuishi vya Iringa – Mufindi (1) na Mbeya – Rungwe (1) umewasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya upekuzi.
