VIFAA 2,400 VYA KUPIMA AFYA VYATOLEWA

 

VIFAA 2,400 VYA KUPIMA AFYA VYATOLEWA

VIFAA 2,400 VYA KUPIMA AFYA VYATOLEWA

DAR ES SALAAM
Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za  Magonjwa yasiyoambukiza katika ngazi ya Msingi, ambapo  imewezesha vituo vya afya 711 kwa kuvipatia vifaa vikiwemo, vifaa vya kupima shinikizo la juu la damu mashine 700, kupima sukari mashine 700, vitendanishi 300 kwa kila kituo na vifaa vya kupima saratani ya mlango wa kizazi 700. 
Aidha, jumla ya watumishi 2,890 kutoka Halmashauri 184 walipatiwa mafunzo kuhusu kugundua na kutibu magonjwa yasiyoambukiza.
Kutokana na mafunzo hayo kumekuwa na ongezeko la kugundua magonjwa yasiyoambukiza ambapo wagonjwa 4,097,319 waligunduliwa ikilinganishwa na wagonjwa 3,742,141 waliogunduliwa mwaka 2022/23 na wote walipata ushauri na matibabu.