2023/2024 AFYA ILIPEWA TSH TRIL 1.2+

 

20232024 AFYA ILIPEWA TSH TRIL 1.2+

2023/2024 AFYA ILIPEWA TSH TRIL 1.2+

DODOMA
Katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali iliipatia Wizara ya afya jumla ya kiasi cha Shilingi 1,235,316,516,000 ili kutekeleza majukumu yake. 
Kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi 502,951,909,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 732,364,607,000 ni kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. 
Aidha, kati ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, kiasi cha Shilingi 148,609,423,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Shilingi 354,342,486,000 ni kwa ajili ya Mishahara ya watumishi wa Wizara makao Makuu, Hospitali ya Taifa, Hospitali Maalum, Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa. Vilevile, kati ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, kiasi cha Shilingi 430,298,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 302,066,607,000 ni fedha za nje