TSH BIL 103 ZABORESHA UTENDAJI MSD

 

TSH BIL 103 ZABORESHA UTENDAJI  MSD

TSH BIL 103 ZABORESHA UTENDAJI  MSD

TANZANIA
Serikali imepeleka MSD kiasi cha Shilingi 103,333,333,343.67 sawa na 50.3% ya bajeti ya Shilingi 205,000,000,000 iliyoidhinishwa kwa ajili ya ugharamiaji wa mnyororo mzima wa upatikanaji wa bidhaa za afya. 
Aidha, vituo vya kutolea huduma za afya kupitia fedha za uchangiaji vimepeleka MSD kiasi cha Shilingi 57,528,128,119.49 na kufanya jumla ya fedha zilizopelekwa MSD kwa ajili ya ugharamiaji wa bidhaa za afya kufikia Shilingi 160,861,461,463.16.
Pia katika kuijengea uwezo MSD kuwa na dawa na bidhaa za afya, Serikali imetoa nyongeza ya jumla ya Shilingi 100,000,000,000 ikiwa ni sehemu ya mtaji wa MSD kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa dawa nchini.
Kupatikana kwa fedha hizo kumewezesha upatikanaji wa bidhaa za afya za kipaumbele aina 290 kuongezeka kutoka wastani wa 73% kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 hadi kufikia wastani wa 79% katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya kufikia Machi 2024