UJENZI WA RMRCC WAFIKIA 26%
MWANZA
Hadi kufikia Machi, 2024 ujenzi wa Kituo Kikuu cha Kikanda cha Uratibu wa Masuala ya Utafutaji na Uokoaji katika Ziwa Victoria (Regional Maritime Rescue Coordination Centre - RMRCC) umefikia asilimia 26.
Lengo la ujenzi wa kituo hiki ni kuboresha usalama wa usafiri katika Ziwa Victoria kati ya nchi ya Tanzania na Uganda chini ya uratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria.
