FILAMU YA AMAZING TANZANIA KUZINDULIWA LEO MEI 15
CHINA
FILAMU mpya ya kuitangaza Tanzania iitwayo ‘Amazing Tanzania’iliyomshirikisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Ali inatarajiwa kuzinduliwa rasmi leo Mei 15 jijini Beijing, China, baada ya uzinduzi wa filamu hiyo Beijing, itaoneshwa katika miji ya Shanghai na Guangzhou, China.
Filamu hiyo, imechezwa pia na Mchezaji Filamu nguli kutoka nchini China ajulikanaye kwa jina la Jin Dong na imefanyika katika maeneo ya Zanzibar na hifadhi ya Arusha ambako kuna maeneo yamefanywa na Rais Samia na mengine Dk Mwinyi.
Aidha lugha zilizotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili, Kiingereza na Kichina pia itakuwa na maudhui mapya badala ya kuwa na mtangazaji kama ilivyokuwa Royal Tour, hii itakuwa na msanii Jin Dong ambaye atapitishwa na Rais Samia katika maeneo mbalimbali ya utalii nchini.
