RADA ZAIDI KUFUNGWA KUIPA NGUVU TMA
MBEYA
Serikali kupitia (Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania -TMA )imekamilisha ufungaji wa rada za hali ya hewa katika mikoa ya Kigoma na Mbeya na kufikisha jumla ya rada tano (5) za hali ya hewa nchini.
Aidha, utengenezaji wa rada nyingine mbili (2) unaendelea na zinatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2024 na zitafungwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Dodoma.
Kumbuka Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea na utoaji wa huduma na kuratibu shughuli za hali ya hewa nchini kwa kutoa utabiri wa kila siku, wa siku kumi na ule wa muda mrefu pamoja na tahadhari ya matukio ya hali mbaya ya hewa ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.
