UJENZI BWAWA LA FARKWA KUANZA SEPTEMBA 2024

 

UJENZI BWAWA LA FARKWA KUANZA SEPTEMBA 2024

UJENZI BWAWA LA FARKWA KUANZA SEPTEMBA 2024

DODOMA
Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Farkwa linalotarajia kuhudumia wananchi wa Jiji la Dodoma na Miji ya wilaya za Chemba, Bahi na Chamwimo unatarajia kuanza mapema mwezi Septemba 2024.
Ujenzi wa Bwawa la Farkwa awamu ya kwanza unafanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kwa gharama ya takribani  shilingi 338,895,000,000
Mradi huo unahusisha ujenzi wa mtambo wa kutibu maji ambao utawezesha uzalishaji wa maji lita milioni 128 kwa siku.