TSH TRIL 9.18 ZAIDHINISHWA UTUMISHI WA WALIMU
TANZANIA
Katika mwaka 2023/24 serikali kupitia TAMISEMI Fungu Namba 56, Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu Namba 02 na Mafungu 26 ya mikoa yakijumuisha halmashauri 184 yaliidhinishiwa bajeti ya shilingi trilioni 9.18.
Kati ya fedha hizo,shilingi trilioni 3.52 ni Fedha za Maendeleo na shilingi trilioni 5.65 ni za Matumizi ya Kawaida, yakijumuisha Mishahara,shilingi trilioni 4.59 na Matumizi Mengineyo ni shilingi trilioni 1.06.
Aidha hadi Machi, 2024 Mafungu 28 yamepokea na kukusanya shilingi trilioni 6.99 sawa na 76.18% ya fedha zilizoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 4.47 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida yakijumuisha Mishahara shilingi trilioni 3.66 na Matumizi Mengineyo shilingi bilioni 810.77. Aidha, shilingi trilioni 2.52 ni fedha za Miradi ya Maendeleo ikijumuisha shilingi trilioni 2.06 Fedha za Ndani na shilingi bilioni 456.39 Fedha za Nje.
kati ya fedha zilizopokelewa shilingi bilioni 848.14 ni za mapato ya ndani ya halmashauri ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 501.98 zimetumika kwenye Matumizi Mengineyo na shilingi bilioni 226.05 zimetumika kwenye Miradi ya Maendeleo
