TSH BIL 96+ ZATUMIKA KWENYE UKIMWI, TB,MALARIA
TANZANIA
Kiasi cha shilingi 96,926,989,204.68 kilitolewa na serikali kwenda wizara ya afya katika mwaka wa fedha 2023/24 kutoka vyanzo vya nje,kupitia mfumo wa D-Fund kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi Misonge ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.
Kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi 73,735,718,410.08 kutoka Mfuko wa Dunia “Global Fund” ilikuwa ni kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, kiasi cha Shilingi 17,073,866,385.60 kutoka Benki ya Dunia na kiasi cha Shilingi 6,117,404,409 kutoka Susan Thompson Buffet Foundation Account kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Programu ya Uwekezaji wa Afya ya Mama na Mtoto.
