TSH BIL 89+ KUIMARISHA UBINGWA BOBEZI
DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga kiasi cha shilingi 89,858,609,000 kwa ajili ya kuimarisha huduma za Matibabu ya Ubingwa na Ubingwa Bobezi hapa nchini kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Serikali inakusudia kuendelea kutoa huduma za matibabu ya Ubingwa na Ubingwa Bobezi katika Hospitali ya Taifa (Muhimbili), Hospitali Maalum, Kanda na Mikoa pamoja na kuanzisha huduma mpya kulingana na mahitaji yaliyopo.
Fedha hizo zitaenda kwenye matumizi ya upandikizaji wa figo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa ya Bungando, upandikizaji wa ujauzito kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma
Aidha Serikali inakusudia kuwekeza kwenye vifaa tiba vitakavyowezesha utoaji wa huduma za ubingwa na ubingwa bobezi ikiwemo ununuzi wa mtambo wa kupima na kutibu moyo (Cathlab) kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na kuendeleza ujenzi wa miundombinu katika Hospitali sita (6) za Rufaa za Kanda za Chato, Mtwara, Mbeya, KCMC, Bugando, Benjamin Mkapa, ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi Kigoma na Hospitali 28 za Rufaa za mikoa
Eneo jingine linalotarajiwa kuimarishwa na serikali ni uboreshaji wa utolewaji wa huduma za ubingwa na ubingwa bobezi na kuendeleza ujenzi wa kituo cha matibabu ya Saratani tawi la Taasisi ya Saratani Ocean Road Mbeya, kuanzisha tawi la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Kanda ya Ziwa (JKCI Chato)
