TSH BIL 75 ZABORESHA UTENDAJI W/MADINI
TANZANIA
Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, serikali kuu iliipatia wizara ya madini kais cha shilingi 75,907,393,763.15 kwa ajili ya kukamilisha usanifu wa jengo la Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), ununuzi wa magari,kugharamia mihadi ya kisheria (Deed of Settlement) kati ya Serikali na Kampuni ya Winshear Gold Corporation na kuwajengea uwezo watumishi wa TGC na watendaji wa Wizara katika shughuli za uongezaji thamani madini.
