MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI YABORESHWA
DODOMA
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji ambapo katika mwaka 2022/2023 ilianza ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji yenye jumla ya hekta 95,005 na katika mwaka 2023/2024 ilianza ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji yenye jumla ya hekta 161,180.46.
Miradi hiyo ikikamilika itaongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 256,185.46 hivyo kufanya eneo linalomwagiliwa kufikia jumla ya hekta 983,466.06 ambazo ni sawa na 81.95% ya lengo la hekta 1,200,000 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 - 2025.
